Translate

Friday, September 22, 2017

Aya ya Leo - Allah


Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.  

It is He who has sent His Messenger with guidance and the religion of truth to manifest it over all religion, although they who associate others with Allah dislike it.(9:33)
Jumaa Mubarak!
 

Thursday, September 21, 2017

Happy New Islamic Year 1439!

Happy New Islamic Year!
Alhamdulillah!
Yeeeh! We made it, we are still here by the grace of Allah! 
If you lost a loved one in the past year, May Allah grant them Janna.
If 1438 was a trial for you, May Allah make this year easier for you.
Lets not forget to pray for all our brothers and sisters facing trials and tribulations right now, May Allah Protect them.
Don't get tired of praying, Keep your faith Strong and May Allah guide and protect us this year and the many more years to come. 
Aaamin!

Friday, September 15, 2017

Aya ya Leo - Nuru (The light)


Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.
 
They want to extinguish the light of Allah with their mouths, but Allah refuses except to perfect His light, although the disbelievers dislike it.(9:32)
Jumaa Mubarak!

Friday, September 8, 2017

Aya ya Leo - Misikiti (Masjid)Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.
The mosques of Allah are only to be maintained by those who believe in Allah and
the Last Day and establish prayer and give zakah and do not fear except Allah,
for it is expected that those will be of the [rightly] guided.
(9:18)
Ijumaa Njema!

Friday, August 25, 2017

Aya ya Leo - Nyumba ya Kwanza ya Ibada (The First House of Worship)


Kwakweli, nyumba ya kwanza (ya Ibada) iliyotengezwa kwajili ya walimwengu ni ule wa Makkah - wenye baraka na muongozo wa ulimwengu.

Indeed, the first House [of worship] established for mankind was that at Makkah - blessed and a guidance for the worlds. (Qur'an 3:96)

Wednesday, August 23, 2017

The Facilities Management Team of Masjid Al-Haram

Appreciating their hard work. May Allah Reward them and bless their families.

No Laziness here, even the supervisors are out in the field.
May Allah guide and protect our brothers and sisters going for Hajj this year.
Mwenyezi Mungu awaongoze na awalinde ndugu zetu wanaokwenda Haji mwaka huu.

Friday, August 4, 2017

Aya ya Leo - Muda wa Umma (Term of Nations)


Na kila umma una muda wake. Utakapo fika muda wao basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia. 

And for every nation is a [specified] term. So when their time has come, they will not remain behind an hour, nor will they precede [it].(Qur'an 7:33)

Friday, July 7, 2017

Aya ya Leo - Mapenzi ya Mali (The love of wealth)

Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema.

It has been made attractive for people to love the desired things; that is, women, children, hoarded heaps of gold and silver, branded horses, cattle and tillage.That is an enjoyment of the worldly life; but with Allah lies the beauty of the final resort. (Qur'an 3:14)

Jumaa Mubarak!

Friday, June 30, 2017

Aya ya Leo - Qur'an


Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.

He is the One who has revealed to you the Book(the Qur'an). Out of it there are verses that are Muhkamat(of established meaning), which are the principal verses of the Book, and some others are Mutashabihat (whose definite meanings are unknown). Now those who have perversity in their hearts go after such part of it as is mutashabih, seeking (to create) discord, and searching for its interpretation (that meets their desires), while no one knows its interpretation except Allah; and those well-grounded in knowledge say:"We believe therein; all is from our Lord." Only the men of understanding observe the advice. (Qur'an 3:7)

Ijumaa Njema


Tuesday, June 27, 2017

Mariam Nabatanzi from Uganda Gave birth to 44 Children

When you wonder how our great great great grandmother Hawa( May peace be with her),was able to populate the world, Allah sometimes decides to show us that it can still happen even today.

This is woman is amazing, and may Allah guide her, give her patience and open more doors for her.

How to be a better person - Hamza Yusuf

Lets not forget to fast the first 6 days of Shawwal immediately after Ramadhan.

Friday, June 23, 2017

Aya ya Leo - Eda (Mourning Period)


Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi. Na wanapo timiza eda yao basi hapana ubaya
kwao kwa wanao jifanyia kwa mujibu wa ada. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.

And those who are taken in death among you and leave wives behind - they, [the wives, shall] wait four months and ten [days]. And when they have fulfilled their term, then there is no blame upon you for what they do with themselves in an acceptable manner.And Allah is [fully] Acquainted with what you do.(Qur'an 2:234)

Wednesday, June 21, 2017

Hadithi ya Leo - Taraweeh
Imehadhithiwa na Abu Huraira:

Nilimsikia Mtume wa Allah akisema kuhusu Ramadhani,"Yeyote aliyesali usiku Kwenye huo mwezi kwa Imani yote na matumaini ya kulipwa na Allah, basi dhambi zake zote zilizopita zita samehewa".

Narrated Abu Huraira:

I heard Allah's Messenger saying regarding Ramadhan, "Whoever prayed at night in it (the month of Ramadan) out of sincere Faith and hoping for a reward from Allah, then all his previous sins will be forgiven."
(Bukhari 2008)

Friday, June 16, 2017

Aya ya Leo - Kumnyonyesha Mtoto (Breastfeeding a baby)

Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.

Mothers may breastfeed their children two complete years for whoever wishes to complete the nursing [period]. Upon the father is the mothers' provision and their clothing according to what is acceptable. No person is charged with more than his capacity. No mother should be harmed through her child, and no father through his child. And upon the [father's] heir is [a duty] like that [of the father]. And if they both desire weaning through mutual consent from both of them and consultation, there is no blame upon either of them. And if you wish to have your children nursed by a substitute, there is no blame upon you as long as you give payment according to what is acceptable. And fear Allah and know that Allah is Seeing of what you do.(Qur'an 2:233)
Jumaa Mubarak!

Aya ya Leo - Imani (Belief)


Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake.

Na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.

The Messenger has believed in what was revealed to him from his Lord, and [so have] the believers. All of them have believed in Allah and His angels and His books and His messengers, [saying], "We make no distinction between any of His messengers." 

And they say, "We hear and we obey. [We seek] our forgiveness, our Lord, and to You is the [final] destination." (Qur'an 2:285)
Ijumaa Njema!

Wednesday, June 14, 2017

Msomi wa Leo - Ibn Arabī

Abū 'Abdullāh Muḥammad ibn 'Alī ibn Muḥammad ibn `Arabī al-Ḥātimī aṭ-Ṭāʾī, alizaliwa Murcia, Spain tarehe 26 Juli 1165. Ibn Arabi alikuwa ni Mwandishi na Msomi mzuri wa dini.

Alianza elimu yake Seville mwaka 1182-1183. Walimu wake walikuwa ma imaam wa karne ya Almohad na wengine walikuwa ma qadi au khatib. Imaam wake wa dini alikuwa
Sheikh Mohammed ibn Qasim Al-Tamimi wa Morocco.Alimaliza masomo yake Morocco mwaka 1200 chini ya mwalimu wake Yusuf Al-Kumi.

Mwaka 1201, Ibn Arab alienda Hija, na akaishi Makkah kwa muda wa miaka mitatu. Hapo ndo alipoanza kuandika kazi yake ya Al-Futuhat al-Makkiyaa.
Baada ya kukaa Makka, alitembelea sehemu nyingi za Syria, Palenstine, Iraq,Anatolia, Baghdad na Madina. Ibn Arabi aliandika vitabu vyake Tanazzulāt al-Mawṣiliyya, Kitāb al-Jalāl wa’l-Jamāl na Kunh mā lā Budda lil-MurīdMinhu, alipoenda kutembelea Mosul na kufunga Ramadhani yake hapo.

Ibn Arabi aliendelea na safari zake na akatembelea Jerusalem, Makka, Misri, Aleppo na Damascus. Mwishoni alirejea Makka ambako aliendelea masomo yake na kudandika kwa muda wa miaka 4 hadi 5, na ni kwenye hii miji ndipo pia alikuwa akifanya ziara ya vitabu vyake. Alifariki dunia tarehe 8 Juli 1240.

Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na amlaze mahali pema peponi.

Tuesday, June 13, 2017

Aya ya Leo - Sala (Prayer)

Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea).

Maintain with care the [obligatory] prayers and [in particular] the middle prayer and stand before Allah, devoutly obedient.(Qur'an 2:238)

Sunday, June 11, 2017

Aya ya Leo - Riba(Interest)

Wale wanaokula riba hawatasimama [Siku ya Kiyama] ila kama anavyo simama anayepigwa na Shetani mpaka kuchanganyikiwa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.
Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

Those who consume interest cannot stand [on the Day of Resurrection] except as one stands who is being beaten by Satan into insanity. That is because they say, "Trade is [just] like interest." But Allah has permitted trade and has forbidden interest. 
So whoever has received an admonition from his Lord and desists may have what is past, and his affair rests with Allah . But whoever returns to [dealing in interest or usury] - those are the companions of the Fire; they will abide eternally therein. (Qur'an 2:275)

Saturday, June 10, 2017

Aya ya Leo - Wealth (Mali)

Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia.
Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.

The example of those who spend their wealth in the way of Allah is like a seed [of grain] which grows seven spikes; in each spike is a hundred grains.
And Allah multiplies [His reward] for whom He wills. And Allah is all-Encompassing and Knowing.
(Qur'an 2:261)

Friday, June 9, 2017

Aya ya Leo - Mkopo kwa Allah (A Loan to Allah)

Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea.

Who is it that would loan Allah a goodly loan so He may multiply it for him many times over? And it is Allah who withholds and grants abundance, and to Him you will be returned.(Qur'an 2:245)

Thursday, June 8, 2017

Qaswida ya Leo kutoka Sweden na mix ya Africa Kusini

Mashaallah! Africa is Beautiful! Alhamdulillah!

Maher has taken his music to another level.
The scenery is beautiful and the Zulu choir Amakhono We Sintu, added a nice touch to the song. Beautiful! Mashaallah!

Aya za Leo - Udanganyifu (Deception)Na katika watu, wako wasemao: Tuna mwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.  Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo.

Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji.
Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.

And of the people are some who say, "We believe in Allah and the Last Day," but they are not believers.They [think to] deceive Allah and those who believe, but they deceive not except themselves and perceive [it] not. In their hearts is a disease, so Allah has increased their disease; and for them is a painful punishment because they [habitually] used to lie.

And when it is said to them, "Do not cause corruption on the earth," they say, "We are but reformers."
Unquestionably, it is they who are the corrupters, but they perceive [it] not. (Qur'an 2:8-2:12)

Tuesday, June 6, 2017

Al Hikma Inawaletea Mashindano Ya Quran

Mwezi wa Qur'ani, jamani I love it, Quran competitions all over the place.
Jamani Hii siyo ya kukosa, sheikh Sudais in Dar? What a treat.
Mashindano ya Qur'an yatakuwa uwanja wa taifa, fanyeni muende, kiingilio ni bureee.
Ukitaka kumjua Sheikh Sudais, soma hii posta yangu ya nyuma ya msomi wa leo.
Alafu msisahau kwenda na ya diamond jubilee hall pale kwenye mashindano madogo yake ya Qur'an ya bi Aisha Sururu foundation.

Monday, June 5, 2017

Aya ya Leo - Ukweli na Uongo (Truth and Lies)

Na Usichanganye Ukweli na Uongo au kuficha ukweli wakati unaujua.  

And do not mix the truth with falsehood or conceal the truth while you know [it].
(Qur'an 2:42)

Friday, June 2, 2017

Aya ya Leo - Dua


Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu

Our Lord, and make us Muslims [in submission] to You and from our descendants a Muslim nation [in submission] to You. And show us our rites and accept our repentance. Indeed, You are the Accepting of repentance, the Merciful.
(Qur'an 2:128)
Jumaa Kareem!

Wednesday, May 31, 2017

1st Makkah Iftaar Ramadhan 1438 ~ Adhaan by Sheikh Fallaatah

Hadithi ya Leo - Qur'an (Al-Baqara na Al-Imran)
Abu Umama alisema alimsikia Mtume wa Allah (S.A.W) akisema:

Soma Qur'ani, kwani siku ya kiyama itakuja kama mwombezi kwa wale wanaoisoma. Some zile mbili zenye mwanga Al-Baqara na Surah Al Imran, kwani siku ya kiyama zitakuja kama mawingu mawili au vivuli viwili au makundi mawili ya ndege, kuwaombea wale waliokuwa wanazisoma. Soma Surah Al-Baqara, kwani kuikimbilia ni baraka na kuikatia tamaa ni chanzo cha huzuni, na waganga hawawezi kukabiliana nayo.

Abu Umama said he heard Allah's Messenger (S.A.W) say:

Recite the Qur'an, for on the Day of Resurrection it will come as an intercessor for those who recite It. Recite the two bright ones, Al-Baqara and Surah Al 'Imran, for on the Day of Resurrection they will come as two clouds or two shades, or two flocks of birds in ranks, pleading for those who recite them. Recite Surah al-Baqara, for to take recourse to it is a blessing and to give it up is a cause of grief, and the magicians cannot confront it. (Mu'awiya said: It has been conveyed to me that here Batala means magicians.)
(~Muslim Book 6, Hadith 302)

Friday, May 26, 2017

Vitu vitano vitakavyo kufanikishia Funga Yako (Ramadhan Tips)

1. Usile chakula kingi. (Gawa utombo sehemu tatu. 1/3 Maji, 1/3 Chakula, 1/3 ya kuhema)
2. Toa Sadaka kila siku kidogo kidogo. Ata ile kufuturisha kila siku pia ni sadaka.
3. Sali sala tano kila siku. Sala 5 zimelazimishwa na zina uzitu kuliko Salaa ya taraweeh ambayo ni sunna.
4. Soma Qur'an kwa utaratibu ili uweze kuilewa.
5.Kuwa na uamko wa Allah (Mcha Mungu). Hii itakusaidia usitende madhambi, kwa kuichunga nafsi yako na maovu.

Ramadhan Kareem Everybody! You got this.

Bosnia 1992: The Omarska Camp - Al Jazeera World

As we start this Ramadhan, let us remember our brothers and sisters that were massacred in the Omarska concentration camp in Bosnia. 
May Allah grant them eternal peace and elevate them to the highest of his heavens. 

Tuesday, May 23, 2017

Africa Uncovered - Mauritania: Fat or Fiction - 11 Aug 08 - Part 2

Well if they knew about processed foods, they wouldn't need to force feed anybody, the fat will come naturally. Okay jokes aside, real issues happening today, get educated.

Friday, March 24, 2017

Fish with Artistic Skills!

And here we thought the human beings are the only artistic beings on earth. How little do we know of God's creation. 

Jumaa Mubarak!

Friday, March 17, 2017

Aya ya Leo Mzigo(Burden)


Na mbebaji mzigo hata beba mzigo wa mwingine. Na aliye zidiwa na mzigo wake aki muomba mwingine amsaidie, hauto punguzwa, ata kama ni ndugu yake wa karibu. Unaweza kuwaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. 

And no bearer of burdens will bear the burden of another. And if a heavily laden soul calls [another] to [carry some of] its load, nothing of it will be carried, even if he should be a close relative. You can only warn those who fear their Lord unseen and have established prayer. And whoever purifies himself only purifies himself for [the benefit of] his soul. And to Allah is the [final] destination. (Qur'an 35:18)


Jumaa Mubarak!


Thursday, March 16, 2017