Translate

Thursday, July 10, 2014

Chakula Bora cha Leo - Ndizi Mbivu


Ndizi kwa sisi wabongo, tunaweza kusema ni dessert. Si unajua hizi desturi za ma keki na cream for dessert, sio style yetu tumeletewa tu, sisi ni matunda kwa kwenda mbele.  Ndizi inafaida nyingi sana, nitajaribu kuzi orodhesha hapa.
1. Ina tryptophan ambayo hubadilika kuwa seratonin, hii husaidia kukuweka kwenye mood nzuri
2. Inazuia Misuli isiji kaze
3. Ina jenga mifupa.
4.Ina punguza uvimbe wa mwili na inakulinda na kisukari
5.Ina Iron ambayo hujenga damu
6.Ina Potassium ambayo hukulinda na stroke, magonjwa ya moyo, na blood pressure.
7. Inakusadia kulainisha choo
8. Ina saidia kusaga chakula mwilini.
9.Ina saidia na kiungulia na kupooza madonda ya tumbo
10. Ina ondoa homa mwilini

Pia ni nzuri kweli wakati wa kufungulia futari, kabla ya swalaa ya maghribi.
Kuna Sababu manyani wameweza kuishi miaka yote hiyo na hili tunda kama chakula chao cha kilasiku.

Futari Njema!

No comments:

Post a Comment